Wednesday, July 22, 2020

Taharuki: Polisi Aanguka na kufariki Ghafla Ndani ya Benki, Mwili Wafanyiwa Vipimo vya Covid19

Police

Sampuli ya mwili wake ilichukuliwa kufanyiwa vipimo  ikiwemo vya covid. Picha; Hisani.

Afisa huyo wa polisi alikuwa akitapika kabla kuanguka na kufariki

Mwili wake ulichukuliwa na wahudumu wa covid bila kubainika chanzo cha kifo

Sampuli ya mwili wake ilichukuliwa kufanyiwa vipimo  ikiwemo vya covid

Hofu imewagubika wenyeji na wafanyikazi katika benki ya Equity tawi la Makutano baada afisa mmoja wa polisi aliyekuwa akifanya kazi ya ulinzi katika benki hiyo kuanguka na kufariki ghafla Jumanne, Julai 21.

Kamanda wa polisi wa eneo hilo Robinson Mboloi alithiyebitisha kisa hicho alieleza kuwa afisa huyu alikuwa mgonjwa majira ya asubuhi, alitapika kabla kuanguka ghafla na kuaga duania chooni.

What happens when you look at crime by the numbers | Science News ...

Kwa mujibu wa jarida la Nation, tawi hilo zima lilifungwa moja kwa moja na maafisa wa kukabiliana na viusi vya corona kabla ya kuuchukua mwili wa marehemu saa mbili baadaye.

‘’ Afisa huyo alikuwa kazini alipofariki ghafla. Chanzo cha kifo chake hakijabainika, mwili wake ulipelekwa katika hospitali yaMeru Level 5,’’ Mboloi alisema.

Baadaye benki hiyo ilinyunyizwa dawa ya kupunguza makali ya virusi hivyo na wahudumu hao wa covid.

Mkurugenzi wa Afya katika kaunti hiyo John Inanga alieleza kuwa waliitwa kuuchukua mwili huo kutokana na hofu ya maabukizi ya covid19 kwa wenyeji.

‘’ Kutokana na janga la corona, watu wanaogopa kushika maiti, hii ndiyo maana tuliitwa,’’ Inanga alisema.

Visa maambukizi ya corona vimeongezeka maradufu, baadhi wakipatikana na virusi hivo hata bila kuonyesha dalili zozote.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/22/taharuki-polisi-aanguka-na-kufariki-ghafla-ndani-ya-benki-mwili-wafanyiwa-vipimo-vya-covid19/

No comments:

Post a Comment