Wednesday, July 22, 2020

Rais Magufuli ametoa wiki mbili taasisi zinazidaiwa na Suma JKT kulipa haraka deni la Sh.bilioni 11

Rais John Magufuli ameaguza taasisi ambazo zinadaiwa na Suma JKT kulipa deni lao ndani ya wiki mbili la sivyo atawachukulia hatua.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo wakati akizindua jengo la Ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) katika eneo la Njedengwa jijini Dodoma. Ujenzi wa jengo umegharibi hadi sasa Sh bilioni 16.8.

Rais Magufuli amesema Suma JKT wanadai Sh bilioni 11 ambazo ni madeni katika taasisi na kumuagiza Waziri Mkuu kulifuatilia jambo hilo.

“Haiwezekani uwe unalindwa alafu uache kulipa natoa wiki mbili wale wote ambao wanadaiwa kama ni taasisi za umma ama binafsi kulipa,” amesema Magufuli.

Aliongezea kuwa ” Kwa kuwa nitakuwa bado ni Rais wewe nijulishe hata kama nitakuwa kwenye kampeni alafu niwe nimechoka niambie hiyo taasisi iliyogoma iwe ya serikali ama binafsi walipe,”.

 

 



source http://www.bongoleo.com/2020/07/22/rais-magufuli-ametoa-wiki-mbili-taasisi-zinazidaiwa-na-suma-jkt-kulipa-haraka/

No comments:

Post a Comment