Tuesday, July 21, 2020

Mashinji Aambulia Kura 2 Ubunge Kawe

What Mashinji said after Halima Mdee snubbed his handshake - The ...Aliyekuwa katibu mkuu wa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Dkt VIncet Mashinji ameangukia pua kwenye mchakato wa ndani wa kuchagua mgombea ubunge jimbo la Kawe kupitia chama cha mapinduzi (CCM).

Mashinji ambaye alitagaza nia nakuchukua fomu ya kuwania ubunge kwenye jimbo hilo liliongoza na mbunge wa chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Halima Mdee kwa miaka kumi na tano.

Mashinji ameambulia kura mbili (2) tu kwenye mchakato huo wa awali huku zoezi la kuhesabu kura bado likiendelea kuhakikisha anapatika na mshindi atayeweza kuwakilisha chama cha mapinduzi kwenye uchaguzi mkuu mapema mwezi Oktoba.

Watia nia wengine walipo kwenye mchakato wa kuomba kuteuliwa na wajumbe wa jimbo la kawe ni pamoja na Askofu Josephat Gwajima, Fransis Nanai, Kipe Warioba na wengine wengi.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/21/mashinji-aambulia-kura-2-ubunge-kawe/

No comments:

Post a Comment