Thursday, July 23, 2020

Simba Yabanwa Mkwakwani

ImageKlabu ya Simba imelazimishwa suluhu ya bila kufungana kwenye mchezo wa ligi kuu bara dhidi ya wagosi wa kaya klabu ya Coastal Union kwenye mchezo wa 37 wa ligi kuu bara ndnai ya  uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Mchezo huo ulioisaidia Coastal Union  kupanda mpaka nafasi ya 6 kwenye msimamo wa ligi kuu bara uliisha kwa Simba kucheza pungufu baada ya beki wao timu hiyo Pascal Wawa kuonyeshwa kadi nyekundu baada ya kufanyia madhambi mshambuliaji wa Coastal Union Ayoub Lyanga dakika ya 75.

Simba sasa inatarajia kusafiri mpaka mkoani Kilimanajoro kukipiga dhidi ya Polisi Tanzania kwenye mchezo wa kuhitimisha ligi kuu bara msimu wa 2019/20 ambayo imekuwa ligi ya kwanza kuwa na timu 20.

Baada ya mchezo dhidi ya Polisi Simba itajipanga kucheza na Namungo FC kwenye mchezo wa fainali ya kombe la shirikisho mkoani Rukwa kwenye uwanja wa Nelson Mandela  mnamo Agosti mosi.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/07/23/simba-yabanwa-mkwakwani/

No comments:

Post a Comment