Thursday, July 23, 2020

Shiekh Mkuu Dar Amkana Makonda “Kwa Yeye ni Nani Mpaka Nimpigie Kampeni”

Mutfi wa Tanzania Amuombea Dua RC Paul Makonda‏ - Global Publishers

Sheikh mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Alhadi Mussa Salim amekana kuhusika kumpigia kura aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kwenye mchakato wa awali wa kuchagua mgombea wa ubunge jimbo la Kigamboni.

Akizungumza jijini Dar es salaam leo Julai 23, 2020 Alhadi Salim Mussa amesema taarifa hizo zilizokuwa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii sio za kweli na ni za kupuuzwa.

“Mimi nitajuaje wajumbe wa mkutano wa wilaya wanaopiga kura na Kama kuna muislam mwenye ushahidi wa namba yangu ikiingia kwake kuelekeza ampigie kura Makonda alete ushahidi kwani Makonda ni nani mpka tutumie dini zetu kumpigia kampeni kuwa achaguliwe niwatake wa Tanzania wapuuze taarifa hizo za uongo”amesema Alhadi.

Mapema Julai 20, 2020 Aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam alianguka kwenye kura za maoni za kuchaguliwa kuwa mgombea wa ubunge jimbo la Kigamboni baada ya kupata kura 112.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/23/shiekh-mkuu-dar-amkana-makonda-kwa-yeye-ni-nani-mpaka-nimpigie-kampeni/

No comments:

Post a Comment