Thursday, July 23, 2020

Ali Kiba Apita Njia Za Diamond

Ali Kiba – Dodo | GetMzikiMapema Disemba 29,2019, Mwanmuziki Diamond na kundi lake la Wasafi pamoja na wasanii kadhaa walianza safari ya siku tatu kwenda mkoani Kigoma kwa njia ya treni na kufanikisha kukodi behewa kadhaa za treni kwa ajili ya safari hiyo kwenda kwenye tamasha la kurudi nyumbani kwa msanii Diamond.

Mwanamuziki mwingine anayefanya vizuri kwenye kiwanda cha Bongo Fleva Ali kiba anatarajia kuanza safari ya kwenda kufanya onyesho lake mkoani Kigoma na ameamua kutumia usafiri wa treni kama alivyofanya Diamond.

Alikiba ambaye pia ametangaza kuukodi behewa maalum kwa ajili ya kusafiri na wasani wenzie huku akiwataka mashabiki wanaopenda kusafiri naye mpaka Kigoma kumuunga mkono kwenye safari hiyo anayoitaka iwe ya kihistori.

Ali ameamua kulipachika jina la Ukarimu bahewa ambalo atalitumia kwenye safari hiyo kwenda kuwafurahisha wana kKigoma manamo Julai 31, 2020.

 

View this post on Instagram

Ewe ndugu yangu, shabiki wangu, mtanzania mwenzangu, mpambanaji mwenye ukarimu, ungana nami kuonyesha ukarimu kwa wakimbizi ambao Tanzania inawahifadhi kwenye kambi za wakimbizi KIGOMA kwa kuchangia chochote ambacho umejaaliwa ambacho kitakuwemo kwenye #BehewaLaUkarimu litakaloenda Kigoma. Kama una shati, tshirt, shuka, mchele, maharage,mafuta, mahindi, chumvi, taulo za kike (sanitary pads), godoro, au chochote. Mimi na wasanii wenzangu ambao tutaenda Kigoma tarehe 31 Mwezi huu tutakuwepo Jumamosi na Jumapili pale Clouds Media Mikocheni kupokea sadaka kwa ajili ya ndugu zetu walio katika kambi za wakimbizi. Homecoming Concert, na #BehewaLaUkarimu lipo kwa ajili ya wenye uhitaji. Kwa ambao mpo mbali mnaweza kuwasilisha michango yenu kupitia namba +255719655554 #HomeComingConcert #BehewaLaUkarimu #Naiaminia255 #JamhuriYaWakarimu #KingKiba

A post shared by alikiba (@officialalikiba) on



source http://www.bongoleo.com/2020/07/23/ali-kiba-apita-njia-za-diamond/

No comments:

Post a Comment