Thursday, July 23, 2020

Mwanafunzi wa darasa la kwanza aungua kwenye sufuria lenye chai akiwa shule na kufariki jijini Dar

Mwanafunzi, Nazia Samweli, mwenye umri wa miaka sita ameunga kwa chai ya moto akiwa shule na kufariki dunia

Mwanafunzi huyo ambaye anasoma darasa la kwanza katika shule ya msingi ya St Anne Maria iliyopo Mbezi kwa Msuguli jijinj Dar es Salaam.

Ilidaiwa kuwa mwanafunzi huyo alifariki baada ya kusukumizwa na wanafunzi wenzake kwenye sufuria yenye chai ya moto.

Kwa mujibu wa taarifa tulizopatiwa ni kwamba mtoto hiyo akiwa kwenye foleni ya kupatiwa chai alisukumwa na wenzake kwa bahati mbaya na kuangukia kwenye sufuria la chai.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/23/mwanafunzi-wa-darasa-la-kwanza-aungua-kwenye-sufuria-lenye-chai-akiwa-shule-na-kufariki-jijini-dar/

No comments:

Post a Comment