Wednesday, July 22, 2020

Rais Magufuli: Nipo tayari kutoa ushirikiano mzuri kwa vyama vyote vya siasa

Rais John  amesema Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu ni wa aina yake utakuwa wa huru na yupo tayari kutoa ushirikiano mzuri kwa vyama vyote vya siasa nchini.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo wakati akizindua jengo la Ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) jijini Dodoma.

Rais Magufuli amewaomba wanasiasa kuhakikisha uchaguzi wa mwaka huu unakuwa ni uchaguzi wa aina yake na kuwataka kufanya kampeni kwa kwa upole, kwa kumtanguliza Mungu, kwa kujua sisi ni taifa la Tanzania, kwa kujenga umoja wa taifa na kunadi sera  kwa wananchi na waweze kuzipima.

“Wasitupime kwa ajili ya matusi mimi ninamaini tukienda hivyo uchaguzi huu utakuwa huru sana na niwahakikishie viongozi wa siasa mimi ni mwenzenu tunajenga nyumba moja na nyumba hiyo tunayoijenga ni Tanzania nawataka kuwathibitishia nitatoa ushirikiano mzuri sana kwa vyama vyote ili tuende na maadili yetu kama tulivyofundishwa na baba wa taifa Mwalimu Julias Nyerere,” amesema Rais Magufuli.

Aidha, ameitaka  Tume ya kusimamia uchaguzi kuzingatia sheria na taratibu za uchaguzi  na vyama vya siasa kuepuka vurugu kwa kuwa vurugu hazijengi.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/22/rais-magufuli-nipo-tayari-kutoa-ushirikiano-mzuri-kwa-vyama-vyote-vya-siasa/

No comments:

Post a Comment