Wednesday, July 22, 2020

Mama Amuua Mpenzi wa Zamani kwa Njia ya Kutatanisha Kabla Kujiwasilisha kwa Polisi

Books to Read If You Love True Crime | Penguin Random House

Jamaa huyo alifariki nyumbani humo kwa Njeri baada ya kuvuja damu kupitia kiasi. Picha: Hisani

Mary Wambui na rafikiye Ann Wanjiru walijiwasilisha kwa polisi baada ya kumuua Anthony

Walitekeleza unyama huo Julai 18, kabla kufika kituoni kupiga ripoti

Mume huyo alifariki katika nyumba ya Njeri kufuatia majeraha mabaya ya visu

Maafisa wa polisi katika kituo cha Ruai wanamzuilia mama mmoja anayedaiwa kumuua mpenziwe wa zamani katika nyumba ya rafikiye ambako mume huyo alimtembelea.

Mary Wambui pamoja na Ann Wanjiru Njeri walijiwasilisha katika kituo cha polisi cha Ruai  Julai 18 baada ya kutekeleza unyama huo nyumbani kwa Njeri kama njia ya kukwepa hasira ya umma.

Gang kills Israeli man in Trans Nzoia County, wife seriously ...

korti ilitoa agizo la kuzuiliwa wawili hao kwa siku 10 zaidi kukamilika uchunguzi. Picha: Hisani

Kwa mujibu wa jarida la Nairobi News, Jamaa huyo alifariki nyumbani humo kwa Njeri baada ya kuvuja damu kupitia kiasi. Hii ni baada ya wawili hao kushirikiana na kumvamia mume huyo kwa kumdunga visu mara kadhaaa.

Inadaiwa kuwa Anthony na Wambui walikuwa wametengana kwa muda lakini mume huyo angali alikuwa na mazoea ya kumtembelea hivyo kumfanya Wambui kuhamia nyumbani kwa rafikiye.

Courts stops TSC from suspending 221 teachers over new curriculum ...

Wawili hao waliwasilishwa katika mahakama ya Makadara ambako korti ilitoa agizo la kuwazuia kwa siku 10 zaidi kukamilika uchunguzi.

Hakimu Mkuu Justice Opondo aliwaamrisha wawili kufanyiwa ukaguzi wa ubongo huku mwili wa marehemu ukifanyiwa upasuaji kubaini chanzo cha kifo.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/22/mama-amuua-mpenzi-wa-zamani-kwa-njia-ya-kutatanisha-kabla-kujiwasilisha-kwa-polisi/

No comments:

Post a Comment