Wednesday, July 22, 2020

Rais Magufuli amevitaka vyombo vya dola kuacha kutumia nguvu na wanasiasa wasiwachokoze

Rais John Magufuli ameviagiza vyombo vinavyosimamia haki kuwa wavulivu wasitumie nguvu sehemu ambayo haihitaji nguvu.

“Niviombe vyombo vya kusimamia haki ikiwemo vyombo vyetu vya dola vituvumilie kidogo visitumie nguvu mahali ambapo hapaitajiki kutumia nguvu,” amesema Rais Magufuli

Aliongezea kuwa “Lakini niwaombe na ninyi wanasiasa msiwachokoze  walinda amani, msiwafanye wakatumia nguvu pahali ambapo ninyi mmewataka kutumia nguvu kwa hiyo sisi sote vyama vyote na mimi nina uhakika tukimtanguliza Mungu katika kampeni tutafanya vizuri na kwa amani,”.

Rais Magufuli amesema kwa sasa wapo huru kwani ratiba imeshatangazwa huu ndio wakati wa kuanza kujinadi na atakayeshinda wanaanza kazi .

“Kwa sasa hivi ni ruksa kila mmoja akafanye kampeni zake kwa uhuru na uwazi akahubiri vizuri na kuzinadi sera zake,” amesema



source http://www.bongoleo.com/2020/07/22/rais-magufuli-amevitaka-vyombo-vya-dola-kuacha-kutumia-nguvu-na-wanasiasa-wasiwachokoze/

No comments:

Post a Comment