Wednesday, July 22, 2020

Rais Magufuli: Hili jengo sio la Sh milioni 143 mimi nimejenga kama hili kwa Sh milioni 40 mmepigwa hadi nyie Takukuru

Rais John Magufuli ameshtukia wizi uliopigwa kati ujenzi wa jengo la Taasisi ya Kuzui na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

“Hawa waliojenga jengo hili ambalo nalizindua hapa Dodoma msiwape kazi nyingine nimewashtukia wamewapiga hadi nyie Takukuru,” amesema Rais Magufuli.

Amesema nyumba hiyo sio ya kujengwa kwa Sh milioni 143 “Mimi nimejenga yangu kama hii nimetumia Sh milioni 40 tu nimemuuliza Waziri Mkuu akaniambia angetumia Sh milioni 60,”.

Rais Magufuli kabla ya kuzindua kwa ofisi ya Takukuru Wilaya ya Chamwino mkoania Dodoma amesema jengo hilo analizindua huku moyo ikiwa inamuuma na kwamba ‘Message sent’.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/22/rais-magufuli-hili-jengo-sio-la-sh-milioni-143-mimi-nimejenga-kama-hili-kwa-sh-milioni-40-mmepigwa-hadi-nyie-takukuru/

No comments:

Post a Comment