Wednesday, July 22, 2020

Magufuli Awapasua TAKUKURU “Msijpendekeze Kwangu”

ALICHOFANYA RAIS MAGUFULI LEO IKULU DODOMA, MAMA SAMIA NA WAZIRI ...Rais wa John Magufuli amewata watendaji wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini (TAKUKURU) kuacha kujipendekeza kwake kwa kutaka kujenga ofisi ya taasisi hiyo wilayani Chato.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa majengo ya TAKUKURU mkoani Dodoma leo Julai 22, 2020 kwenye eneo la Ihumwe amesema kitendo cha watendaji wa taasisi hiyo kujenga ofisi si sawa kwakua TAKUKURU wilayani Chato wana ofisi.

“Msijipendekeze kwangu msifanye mambo kwa kunifurahisha mimi mumesema mnataka kujenga jengo la TAKUKURU Chato wakati kule ofisi ipo na mimi nilipokuwa waziri wa ujenzi nilishawapa ofisi pale tena nzuri tu ya gholofa jipendekezeni Chato nikimaliza urais sio sasa hivi” amesema Rais Magufuli.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/22/magufuli-awapasua-takukuru-msijpendekeze-kwangu/

No comments:

Post a Comment