Wednesday, July 22, 2020

Magufuli: Vile vifaa vya Dar mkavichukue unapoanza nyumba mpya haina haja kitanda kiwe kipya mwishowe utasema mke awe mpya

Rais John Magufuli ameipata Ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kiasi cha Sh milioni 500 kwa ajili ya kutatua changamoto zinazowakabili.

“Changamoto zilizobaki nitamuambia Wairi Mkuu afuatilie ninawaongezea Sh milioni 500 mkanunue hivyo vifaa mnavyotaka,”amesema Rais Magufuli.

Aliongezea kuwa “Lakini vile vifaa ambavyo vipo Dar es salaam mvibebe mvilete hapa hakuna sababu unapoanza na nyumba mpya na kitanda lazima kiwe kipya , godoro liwe jipya mwishowe utasema na mke awe mpya kwa hiyo  vile vifaa viletwe na bahati nzuri magari ya kubebea yapo,”.

Amesema wakati mwingine unaweza kuleta vifaa vipya vikawa ni changamoto katika kuwasaidia.

“Kwa sababu tunaingia kwenye uchaguzi vikawa ni vifaa ambavyo vitaharibu information zenu mnazotaka kuzitumia nikuombe Jajji Kaijage vile viti vyako vizuri vya kule Dar es Salaam na zile meza nzuri, mafaili, compyuta msiziache,” amesema Magufuli.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/22/magufuli-vile-vifaa-vya-dar-mkavichukue-unapoanza-nyumba-mpya-haina-haja-kitanda-kiwe-kipya-mwishowe-utasema-mke-awe-mpya/

No comments:

Post a Comment