Thursday, July 9, 2020

Rais Magufuli amemteua Malata kuwa Wakili Mkuu wa Serikali

 

Rais John Magufuli  amemeteua Gabriel Pascal Malata kuwa Wakili Mkuu wa Serikali.

Kabla ya uteuzi huo Malata  alikuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali na anachukua nafasi ya Dk. Julius Clement Mshamba.

Wakati huo huo Rais Magufuli amemteua Dk. Boniface Luhende kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali (Deputy Solicitor General).

Kabla ya uteuzi huo Dk. Luhende alikuwa Mhadhiri wa katika shule kuu ya sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na anachukua nafasi ya Gabriel Pascal Malata ambaye ameteuliwa kuwa Wakili Mkuu wa Serikali.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikuluu, imeeleza kuwa uteuzi wa viongozi hao unaanza leo Julai 10, 2020.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/10/rais-magufuli-amemteua-malata-kuwa-wakili-mkuu-wa-serikali/

No comments:

Post a Comment