Thursday, July 9, 2020

Dondoo za leo: Mgombea urais Zanzibar kutajwa leo je atakuwa ni Dk. Mwinyi?, Rais Magufuli afanya uteuzi na Chadema wamjibu Nassari

Habari ya asubuhi mdau wa Opera News ni siku nyingine ya Alhamisi Julai 09, 2020, matumaini yetu upo salama na karibu katika ujenzi wa taifa.

Tunakukaribusha katika dawati letu la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazopamba asubuhi ya leo.

Habari hizo ni Mgombea urais Zanzibar kutajwa leo hadharani je atakuwa Dk. Mwinyi?, Rais Magufuli amefanya uteuzi kwa DC, Mkurugenzi Mtendaji na Katibu Tawala je unajua ni akina nani wameteuliwa? soma habari hizi kwa kina na mwisho ni Chadema wamemjibu Nassari.

Karibu msomaji wetu;

MGOMBEA URAIS ZANZIBAR KUTAJWA LEO HADHARANI, JE ATAKUWA DK. MWINYI?

Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi  Taifa (NEC) leo inatarajia kumtaja mgombea urais Zanzibar kati ya majina matatu yaliyopendekezwa.

Jana Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa, ilimaza kikao chake na kupendekeza majina matatu ya wagombea wa urais Zanzibar kwa NEC.

Majina hayo yatawekwa wazi leo katika kikao cha NEC kwa wajumbe kwa ajili ya kupiga kura kumchagua mwanachama mmoja kwa nafasi hiyo ya kugombea urais.

Soma zaidi

RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI KWA DC, MKURUGENZI MTENDAJI NA KATIBU TAWALA

Rais John Magufuli amewafanya uteuzi kwa Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji na Katibu Tawala.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana usiku na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa Rais Magufuli amemteua  Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Advera John Bulimba kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nzega mkoani Tabora.

Kabla ya uteuzi huo ACP Bulimba alikuwa kamanda wa Kikosi cha Polisi Tazara na anachukua nafasi ya Godfrey Ngupula.

Soma zaidi

CHADEMA YAMJIBU NASSARI

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkupitia kwa Katibu wa chama hicho mkoa wa Arusha Reginald Massawe kimemjibu aliyekuwa mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki kupitia Chadema Joshua Nassari nakusema alijua hataruhusiwi tena kugombea ubunge katika jimbo la Arumeru Mashariki baada yakushindwa kutekeleza yale aliyoambiwa na chama

“Tarehe 4 mwezi wa saba Mh Nassari alinitumia sms kama katibu wa mkoa akisema Naomba nihakikishie kama nitapita CHADEMA nakupewa nafasi yakugombea ubunge tena,Nasari alijua kabisa tusingempitisha jimbo la Arumeru Mashariki-“Massawe

Soma zaidi



source http://www.bongoleo.com/2020/07/10/dondoo-za-leo-mgombea-urais-zanzibar-kutajwa-leo-je-atakuwa-ni-dk-mwinyi-rais-magufuli-afanya-uteuzi-na-chadema-wamjibu-nassari/

No comments:

Post a Comment