Thursday, July 23, 2020

Sokomoko Jamaaa Akifukua Mwili wa Mkewe Baada ya Kuzikwa kwa Mchumba wa Pili

Mary Akinyi alitengana na John Odhiambo baada ya kuishi naye na kujaliwa watoto saba

Alipata mume wa pili aliyemuaa baadaye na hawakujaliwa watoto

Alifariki na mume huyo wa pili akaamua kumzika

Mume wa Kwanza alifika kortni na kupewa idhini ya kuufukua mwili na kuuzika kwake

Kilitokea kisa cha kustaajabisha katika kaunti ya Migori baada ya Mahakama kumpa jamaa mmoja aliyetambuliwa kama John Odhimbo idhini ya kuufukua mwili wa aliyekuwa mkewe na kumzika tena.

Migori Law Courts, Migori (+254 20 2318775)

Kulingana na mdaku wetu, Kisa hicho kilifanyika katika kijiji cha Rangenya kaunti ya Migori.

Mwanamke huyo alikuwa mkewe John Odhiambo kwa miaka kadhaa na kujaliwa na watoto saba kabla wawili hao kukosana na kutengana.

Baadaye, mama huyu alijaliwa kupata mume wa pili aliyemuoa huku akiacha wanawe saba na mume wa kwanza.

Mama huyo hatimaye aliugua na kufariki, mumewe wa pili alimzika akijua fika kuwa huyo alikuwa mkewe.

La kusikitisha ni kuwa mume wa kwanza wa Akinyi aliposikia kuwa amezikwa kwa mume huyo, alifika kwa mahakama akitaka nafasi ya kuruhusiwa kuuzika mwili wa mkewe.

Huku ndugu za marehemu wakimuunga mkono, mahakama hiyo ilimpa idhini ya kuufukua mwili huo alikozikwa na kumzika tena nyumbani kwake aliko wanawe saba.

‘’Mary ni mke wangu, tuliishi naye kwa miaka kadhaa na tuna watoto saba.  Huyu mume mwengine alimuiba kutoka kwangu. Mwanzo sikujua kuhusu aliko, nilikuwa nikimtafuta. Sasa nimempata na siwezi hu mwili wake kuzikwa mbali nami,’’ Odhiambo alisema.

Mume huyo wa pili alilazimika kutoroka asipatikane huku John Odhiambo na watu wake wakiufukua mwili huo chini ya ulinzi wa polisi tayari kumzika kwake.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/23/sokomoko-jamaaa-akifukua-mwili-wa-mkewe-baada-ya-kuzikwa-kwa-mchumba-wa-pili/

No comments:

Post a Comment