Tuesday, July 21, 2020

Baada Ya Kujizolea Kura 6 Steve Nyerere Awapasua Wajumbe Iringa Mjini

Image

Aliyekuwa mtia nia wa ubunge jimbo la Iringa Mjini Steve Mengere amesema kitendo cha kupata kura kwenye mchakato wa awali wa kuchagua mgombea wa ubunge kupitia CCM hakijamakatisha tamaa na hata kidogo na kimemfanya ajipange zaidi kwenye uchaguzi ujao.

Akizungumza na kituo cha redio cha Clouds Fm baada ya kumalizika kwa zoezi la upigaji kura jimboni humo Mengere amesema wapo watu wengi walio na nyadhifa lakini hawajapata kura hata moja na kulikuwa na ugomvi ndani ya chama hicho kabla ya yeye kutangaza nia.

“Wenyewe kwa wenyewe walikuwa hawaelewani na kulikuwa na magenge mengi ndo maana Msigwa ameaongoza miaka kumi, siwezi kukata tamaa nashukuru sijapata ziro maana wapo watu wakubwa wamepata ziro sembuse mimi niliyekuwa siwajui hata wajumbe”amesema Steve.

Ikumbukwe kuwa mchakato wa awali wa ndani ya chama umeanza jana Julai 20,2020 na utaendelea kwa siku kadhaa kabla ya ngazi za juu za Wilaya na taifa kukaa na kuchagua jina moja.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/21/baada-ya-kujizolea-kura-6-steve-nyerere-awapasua-wajumbe-iringa-mjini/

No comments:

Post a Comment