Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Iringa mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa, amewapongeza wanachama wa kawaida wa Chama cha Mapinduzi kwa kutowachagua waliohamia kwenye chama chao.
“Kwa mara ya kwanza nichukue fursa hii kuwapongeza sana wanachama wa kawaida wa CCM katika maeneo mbalimbali kwa kuwapa walichostahili hawa wahamiaji,” aliandika Msigwa katika ukurasa wake wa Twitter.
Msigwa amesema watu hao hawana msimamo, fadhila wala nidhamu.
“Mmeonyesha jinsi ambavyo mmewapuuza, hongera kwa hilo,”aliandika Msigwa.
Kwa mara ya kwanza nichukue fursa hii kuwapongeza sana wanachama wa kawaida wa CCM katika maeneo mbalimbali kwa kuwapa walichostahili hawa wahamiaji, wataka faida , watu wasio na fadhila,misimamo na wala nidhamu. Mmeonyesha jinsi ambavyo mmewapuuza, Hongera kwa hilo .
— peter msigwa (@MsigwaPeter) July 22, 2020
source http://www.bongoleo.com/2020/07/22/mchungaji-msigwa-awapongeza-wanachama-wa-ccm-kwa-kuwapiga-chini-waliohamia/
No comments:
Post a Comment