Wednesday, July 22, 2020

Huyu Ndiye Mrembo Aliyechukua Nafasi ya Tanasha Donna? Mama Dangote Athibitisha

Tanasha's replacement? Mama Dangote posts photo of hot woman on Instagram

Mama Dangote alichapisha picha ya mwanadada mrembo mtandaoni kwa mara ya kwanza baada ya mwanawe kutengana na Donna

Alikuwa mwanamtindo mrembo kupindukia

Limekuwa jambo la kawaida kuwa kila msanii Diamond anapopata mrembo wa kuchumbia, mamake huwa katika mstari wa mbele kuthibitisha, kutia muhuri na kumpa baraka zake.

View this post on Instagram

👌👌👌

A post shared by Sandrah…! (@mama_dangote) on

Siku chache tu baada ya msanii huyo kueleza bayana kuwa alikuwa amepata kipusa na yupo tayari kumtia pete kwa sherehe ya harusi anapofikisha umri wa miaka 31, Mama Dangote amejitokeza kutupa kionjo cha anayedhaniwa kuwa kipusa huyo mwenye bahati.

Si utani, atakuwa mwenye baraka maana Diamond atakuwa amewaruka zaidi wa warembo watano tajika kumtia pete huyo.

View this post on Instagram

Hi 🌸. @petefarasi9

A post shared by Jihan Dimack (@jihandimack) on

Tamasha iliyoandaliwa na Wasafi ilifunua mabivu na mabichi, mwanamtindo Jihandi Mack akiwaacha wengi vinywa wazi kwa urembo. Si umbo, si rangi, si mavazi, si nywele, si macho, urembo wa Johandi ulinata, Mama Dangote akishindwa kuzuia furaha yake.

Moja kwa moja aliichukua picha yake na kuipachika kwenye ukurasa wake wa instagram huku akimrundia sifa.

View this post on Instagram

💅🏽 @platinumseacliff

A post shared by Jihan Dimack (@jihandimack) on

Je, ni nani asiyejua kuwa Mama Dangote anapomkubali mrembo naye mwanawe hana lingine ila kutia sahihi?

Wengi wafuasi wa Diamond na mamake walijimwaya mtandaoni na kuthibitisha kuwa kweli Jihandi hakuwa na doa wala toa na alikuwa chaguzi bora kuchukua nafasi ya Tanasha Donna.

Msanii Diamond Platnamz walitemgana na Donna Februari 2020 baada ya uhusiano wao kusambaratika licha kufanya kila nia kuukwamua.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/22/huyu-ndiye-mrembo-aliyechukua-nafasi-ya-tanasha-donna-mama-dangote-athibitisha/

No comments:

Post a Comment