Tuesday, July 21, 2020

Dondoo za leo: Marufuku sherehe za kuongoza kura za maoni, Lissu asema waliotaka kumuua bado wanaitwa wasiojulikana na Pacha wa Waziri wa Madini aibuka kidedea kura za maoni

Habari ya asubuhi mdau wa Opera News ni siku nyingine ya Jumatano Julai 22, 2020, matumaini yetu upo salama na karibu katika ujenzi wa taifa.

Tunakukaribusha katika dawati letu la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazopamba asubuhi ya leo.

Habari hizo ni Marufuku sherehe za kuongoza kura za maoni kulikoni?, Lissu asema waliotaka kumuua hadi sasa wanaitwa wasiojulikana na Pacha wa Waziri wa Madini ameibuka kidedea katika uchaguzi wa kura za maoni je unajua ni wapi? soma habari hizi kwa kina.

Karibu msomaji wetu;

MARUFUKU SHEREHE ZA KUONGOZA KURA ZA MAONI

WANAOGOMBEA uteuzi wa nafasi ya ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), wamepigwa marufuku kusheherekea kura walizozipata, na watakaofanya hivyo watakuwa wamekiuka maagizo ya chama na watachukuliwa hatua.

Imeelezwa kuongoza kwenye kura za maoni siyo kwamba mhusika umeteuliwa na CCM kupeperusha bendera ya chama hicho kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, mwaka huu, bali hiyo ni hatua ya awali ambapo majina ya wagombea yatapelekwa kwenye vikao vya Taifa vya chama hicho kupitisha jina la mgombea mmoja.

Hayo yalibainishwa juzi na msimamizi wa uchaguzi wa kura za maoni za ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Joachim Simbila, baada ya kumaliza kutangaza matokeo ya kura za maoni.

Alisema maelekezo ya chama ni marufuku mgombea aliyeongoza kura za maoni kufanya sherehe za aina yoyote, kwa kuwa haijulikani kama jina lake litakuwa limepitishwa kwa ajili ya kupeperusha bendera ya CCM wakati wa uchaguzi mkuu.

Soma zaidi

LISSU: WALE WALIOKUJA  KUNIUA BADO WANAITWA WASIOJULIKANA

Makamau mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleoa (Chadema), Tundu Lissu amesema waliotaka kumuua hadi sasa wanaitwa wasiojulikana maana yake bado wapo na hawajasema kama lengo lao wameliacha.

“Bado kuna hatari ya maisha yangu ninarudi nchini katika mazingira ya hatari dhidi yangu haijaondoka lakini narudi tu ni nyumbani kwetu,” amesema Lissu.

aliongezea kuwa “Ninafahamu kwamba mamilioni yenu mlilia, mliomba Mungu na kujitolea hapa nilipo nina damu ya Watanzania nisiowajua, nina damu ya wakenya nisiowajua kwa sababu niliwekewa damu mara tatu ya ujazo wangu wa kawaida katika hospitalia ya Nairobi,”.

Soma zaidi

PACHA WA WAZIRI WA MADINI AMEIBUKA MSHINDI KURA ZA MAONI

Mgombea Ubunge, Kulwa Biteko ameibuka kidedea katika uchaguzi wa kura za maoni katika jimbo la Busanda kwa kupata kura 665.

Kulwa ambaye ni pacha wa  Waziri wa Madini, Doto Biteko.

Katika uchaguzi huo aliyeshika nafasi ya pili ni Laulencia Bukwimba 94 na watatu ni Abdala Hussein 20.

Soma zaidi

 



source http://www.bongoleo.com/2020/07/22/dondoo-za-leo-marufuku-sherehe-za-kuongoza-kura-za-maoni-lissu-asema-waliotaka-kumuua-bado-wanaitwa-wasiojulikana-na-pacha-wa-waziri-wa-madini-aibuka-kidedea-kura-za-maoni/

No comments:

Post a Comment