Wednesday, July 8, 2020

Mbeya Kumekucha Wazee Wa Kimila Wamchangia Pesa Dkt.Tulia Achukue Fomu Ya Ubunge

ImageBaada ya hapo jana umoja wa wanawake wa chama ha Demokrasia na Maendeleo (BAWACHA) kujitokeza na kumchukukia fomu ya kugombea ubunge wa jimbo la Mbeya mjini Mbunge aliyemaliza muda wake Joseph Mbilinyi.

Leo Julai 8, 2020 kikundi cha wazee wa kimila wilayani Rungwe mkoani humo wamemchangia pesa Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson kwa ajili ya kuchukua fomu ya kugombea ubunge.

Dkt. Tulia ambaye amesema atagombea ubunge kwenye uchaguzi unaokuja amesema atatangaza jimbo la kugombea hivi karibuni huku akiwashukuru wazee hao wa kimila kwa kitendo chao cha kumchangia.

Dkt. Tulia kwa kipindi kirefu amekuwa akihusishwa na kugombea ubunge kwenye jimbo la Mbeya Mjini ambalo lipo chini ya mbunge wa CHADEMA Joseph Mbilinyi ambaye naye ametangaza nia ya kuendelea kugombea kwenye jimbo hilo.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/08/mbeya-kumekucha-wazee-wa-kimila-wamchangia-pesa-dkt-tulia-achukue-fomu-ya-ubunge/

No comments:

Post a Comment