Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya amesema kitendo cha aliyekuwa mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari kujiunga na chama cha Mapinduzi ni bomu kwa wapinzani.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kumpokea iliyofanyika kwenye ukumbi wa CCM Mkoani Arusha,amesema Nassari alikuwa anasumbua sana CCM kutokana na akili zake lakini sasa atausumbua upinzani.
“Mimi nilikuwa diwani hapa Arumeru, kati ya watu waliokuwa wanatupasua kichwa mchana na usiku, wanatunyanyasa, wanatufanya tusilale kwa sababu ya akili yake ya kufyatua yanayotengezwa na CCM alikuwa ni Nassari. Leo bomu limekuja kwetu ligeuzie kwa wapinzani.”amesema Ole Sabaya.
Ikumbukwe kuwa Joshua Nassari amejiunga na CCM ikiwa ni miezi kadhaa baada ya kuvuliwa ubunge na kutokana na kushindwa kuhudhulia baadhi ya vikao vya bunge la 11 mnamo March 19, 2019.
source http://www.bongoleo.com/2020/07/08/dc-sabaya-nassari-ni-bomu/
No comments:
Post a Comment