Wednesday, July 8, 2020

Mamake Diamond Atuma Ujumbe wa Kipekee Baada ya Kuguswa Roho Mwanawe Tanasha Donna

Lover, 38, to Diamond's mother, 50, shares evidence of their ...

Mamake Msanii Diamond Platnamz, Sandra Kassim alishindwa kuficha furaha yake baada ya mpenzi wa zamani wa mwanawe, Tanasha Donna kuchapisha video ya mjukuuwe mtandaoni.

Katika video hiyo, mwanawe Donna anaonekana akitembea kwa mara ya kwanza, kisa kilichomsisimua sana Sandra.

Kulingana na mamake msanii tajika Diamond Platnumz, mtoto huyo, Naseeb Junior alikuwa anasubiri kuanza kutembea siku sawa yeye anaposherekea siku ya kuzaliwa.

‘’Kweli leo nimeonyeshwa surprise na Bwana Naseeb tom kaka kasikia leo mkewe kazaliwa na yy katembea kweli Bwana Naseeb ananipenda anataka aje afurahi na mm Mkewe,’’Aliandika.

Licha ya Diamond na Tanasha Donna kuonyeshana visogo Februari 2020, ni wazi kuwa mamake msanii huyo angali ana uhusiano mkubwa na mjukuu wake.

Mashabiki wa Sandra walijimwaya upesi mitandani kumrundia sifa kwa uhusiano bora kati yake na Tanasha na haswa mjukuu wake.

View this post on Instagram

Kucheka nako K…

A post shared by Sandrah…! (@mama_dangote) on

Uhusiano kati ya Diamond na Donna ulisambaratika  mapema mwakani, Tanasha Donna kwa wakati mmoja akijitokeza na kudai kuwa mamake Mondi ndiye alikuwa chanzo kikuu cha kusambaratika kwa uhusiano huo.

Kulingana na msanii Diamond, uhusiano wake na  Donna uliharibika maana kunayo baadhi ya maswala ya kimsingi ambayo hawakukubaliana kwayo. Aliyasema hayo huku akisisitiza kuwa lengo lake kuu lilikuwa kumfungisha Donna pingu za maisha na hata hakumcheza na mke yeyote walipokuwa wapenzi.na



source http://www.bongoleo.com/2020/07/08/mamake-diamond-atuma-ujumbe-wa-kipekee-baada-ya-kuguswa-roho-mwanawe-tanasha-donna/

No comments:

Post a Comment