Wednesday, July 8, 2020

Nassari Ajiunga Rasmi CCM

LIVE: JOSHUA NASSARI ANAPOKELEWA KWENYE UKUMBI WA CCM MKOA ARUSHA ...Aliyekuwa wahi mbunge wa Arumeru Mashariki (CHADEMA) Joshua Nassari amejiunga rasmi kwenye chama cha mapinduzi (CCM) ikiwa ni mwaka mmoja baada kuvuliwa ubunge kutokana na kushindwa kuhudhuliwa vikao vya bunge.

Nassari ambaye alikuwa mwanachama wa CHADEMA alitangaza kuacha shuguli za siasa baada ya kuvuliwa ubunge  amepokelewa rasmi CCM leo Julai 8, 2020 kwenye ukumbi wa CCM mkoani Arusha na mwenyekiti wa UVCCM Taifa Kheri Denice.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kupokelewa Nassari amesema angeweza kukaa nje na kufanya kazi lakini amerudi nchini kwakua anaipenda nchi yake ndio maana amerejea kutetea nchi anayoipenda.

“Nilishawahi kusema kuwa siku nitakayo kuja kujiunga na CCM nitakuja mchana ili kila mtu anione na nimerudi kwakua naipenda Tanzania, sijaja kwa sababu nataka kitu kutoka huku nimekuja kuitetea nchi yangu” amesema Nassari.

Mapema March 19, 2019 mahakama kuu nchini iliridhia uamuzi wa spika wa Bunge Job Ndugai kumvua ubunge Nassari kutokana na kushindwa kuhudhulia vikao vya bunge.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/07/08/nassari-ajiunga-rasmi-ccm/

No comments:

Post a Comment