Baada ya kufika kileleni, alimuona nyani ambaye alikuwa akimjia tayari kumshambulia. Picha: Hisani.
Dickson Maina alisikia watu wakipiga kamsa akaamua kufika hadi juu la gororofa hilo kuona kilichukuwa kikijiri
Baada ya kufika kileleni, alimuona nyani ambaye alikuwa akimjia tayari kumshambulia
Alijirusha na kuangukia ua la mabati ambalo lilimwacha kwa majeraha ya macho, uso na hata kuvunja mkono
Dereva mmoja amesalia na majeraha mabaya baada ya kuruka kutoka gorofa la nne kumhepa nyani aliyetaka kumshambulia.
Dickson Maina ambaye ni mkaazi wa mtaa wa Kayole ameeleza kuwa aliamua kupanda hadi gorofa ya nne baada ya kusikia watu wakipiga mayowe baada ya kumuona nyani huyo, naye akashikwa na uchu wa kumuona hivyo moja kwa moja akapanda hadi kileleni.
Kutokana na video hiyo iliyosambaa mitandaoni, nyani huyu alianza kumjia Dickson, alipogundua kuwa mnyama huyu alikuwa na nia ya kumvamia, aliruka kujiokoa na hapo akaangukia ua la mabati.
#MindYourOwnBusiness@kwskenya pic.twitter.com/KQqmnqZeeg
— Robin Njogu (@robinnjogu) July 7, 2020
‘’Mabati yalinikata mkono, pia nilivunjika mkono na uso pia una majareha,’’ Maina alisema.
‘’Umati uliokuwa ukimkibiza nyani huyo ulifika haraka kuniokoa na kunipeleka hospitalini,’’ aliongezea.
Maina ambaye alikuwa akisimulia kisa hicho, alieleza kuwa daktari aliyemhudumia alimwarifu kuwa majeraha aliyoyapata hayakuwa mabaya na kuwa atapona karibuni.
Video ya tukio hilo ambalo lilisambaa mitandaoni liliibua hisia mseto, baadhi wakimuonea huruma na kumpa pole huku wengine wakishangaa ni kwanini aliamua kuruka katika hali kama hiyo huku anajua fika kuwa nyani hana uwezo wa kumjeruhi mtu.
source http://www.bongoleo.com/2020/07/08/jamaa-aliyejirusha-kutoka-gorofa-la-nne-kumhepa-nyani-asimulia-kisa-chake/
No comments:
Post a Comment