Shilole Atangaza Kuvunja Ndoa yake Na Uchebe “Alikuwa Ananipiga kila Mara”
Mwanamuziki Zuena Mohammed (Shilole) amevunja ndoa na aliyekuwa mume wake Ashrafu Sadiki (Uchebe) ikiwa ni baada ya miaka miwili ya wawili hao kufunga ndoa kwa kile alichodai kupigwa mara kwa mara na mume wake huyo.
Shilole ametangaza uamuzi huo leo kupita ukurasa wake wa Instagram na kuomba radhi kwa umma kutokana na kushindwa kusema juu ya manyanyaso anayopita kwenye ndoa yake.
“Nimeona nivunje ukimya kwa kuweka wazi kwamba MUME WANGU ASHRAFU SADIKI (UCHEBE) ANANIPIGA SANa, na hata baada ya kunipiga hajali kupiga simu kujua naendeleaje, nauguzwa na watu baki hospitali,na bado manyanyaso mengine yanayoikosesha hii ninayoiita ndoa uhai na furaha”ameandika Shilole.
Ikumbukwe kuwa Shilole na aliyekuwa mume wake Ashrafu walifunga ndoa hiyo jijini Dar es salaam mnamo Disemba 9, 2017 baada ya kudumu kwenye mahusiano kwa kipindi cha takribani mwaka mmoja.
No comments:
Post a Comment