
Aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob amesema uchaguzi ni noma yaani kura mbili zimemfanya Master Jay anyoe rasta zake.
Producer Mkongwe wa Muziki Joachim Marunda Kimaryo maarufu kama ‘Master Jay’ tayari alichukua fomu ya kugombea Ubunge katika Jimbo la Rombo kupitia Chama cha Maoinduzi (CCM).
“Watu wa Rombo mbona wakatili hivyo si mngemuambia kabisa asinyoe rasta zake alizofuga miaka mingi,” aliandika Jacob.
Jacob aliandika ujumbe huo katika ukurasa wake wa Twitter baada ya kupata taarifa Master J amepata kura mbili katika uchaguzi wa kura za maoni jimbo la Rombo.
UCHAGUZI NI NOMAAAAA
Yani Kura 2 Ndiyo zilimfanya Master Jay anyoe Rasta zake?
Watu wa Rombo Mbona wakatili hivyo?
Si Mngemwambia Kabisa Kabla ajanyoa Rasta zake alizofuga Miaka Mingi.— Boniface Jacob (@MayorUbungo) July 21, 2020
source http://www.bongoleo.com/2020/07/21/jacob-uchaguzi-nomaaaa-yaani-kura-mbili-zimemfanya-master-j-anyoe-rasta/
No comments:
Post a Comment