Tuesday, July 21, 2020

Gwajima Angukia Pua Ubunge Kawe

Image

Askofu wa kanisa la ufufuo na uzima Josephat Gwajima ameshindwa kufua dafu kwenye mchakato wa awali wa kutafuta mgombe wa ubunge kwenye jimbo la Kawe kupitia chama cha mapinduzi (CCM) kuelekea kwenye uchaguzi mkuu mapema mwezi oktoba.

Gwajima ambaye amepata kura 79 ameshika nafasi ya tatu nyuma ya Furaha Dominc aliyepata jumla ya kura 101 akifuatiwa na Angela Kiziga aliyejizolea kura 85 huku aliyekuwa meya wa Manisapa ya  Kinondoni Benjamin Sitta akiwa amejikusanyia jumla ya kura 61.

Hatua ya awali mchakato wa kuchagua wagombea wa nafasi ubunge kwenye majimbo mbalimbali nchini inaendelea leo baada ya kufunguliwa rasmi hapo jana Julai 20,2020 kwa vikao vya ndani ya jimbo kabla ya hatua za juu za wilaya, mkoa na taifa kutoa jina la mgombea rasmi.

Jimbo la Kawe lilikuwa na watia nia 170 ambao walijitokeza kwenye mchakato wa kuomba kuteuliwa kuwakilisha bendera ya chama cha mapinduzi kwenye mchakato wa uchaguzi utakaofanyika mapema Oktoba 28.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/21/gwajima-angukia-pua-ubunge-kawe/

No comments:

Post a Comment