Tuesday, July 21, 2020

Boniface Jacob Ampasua Mashinji Baada Ya Kupata Kura 2

MASHINJI MM NI MZIMA SIUMWI - KUSAGA NEWSAliyekuwa meya wa Manispaa ya Ubungo Boniface Jacob ameshangaa kitendo cha aliyekuwa katibu mkuu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Vincet Mashinji kupata kupata kura kura 2 kwenye mchakato wa awali wa kuchagua wagombea wa ubunge jimbo la Kawe.

Boniface ambaye ametuma ujumbe kupitia ujumbe kwenye ukurasa wake wa twitter na kutaka kupewa sababu tatu za kwa nini amepata kura hizo za aibu.

Kwako Mwalimu Kashasha Hii ya huko Kawe,Mtu kutoka Kuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Kikuu cha Upinzani Mpaka Kupata Kura 02 Maana yake Nini? a)CCM haipendi Wasaliti? b) CCM Kawe Wanajua lile Kopo tupu Kichwani? c)CCM kawe haitaki Watu Wenye tamaa tamaa ya ovyo?” ameandika Jacob.

Ikumbukwe bado mchakato wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kusaka wagombea nafasi za ubunge kwenye majimbo mbalimbali kuelekea kwenye uchaguzi mkuu mwezi Oktoba.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/07/21/boniface-jacob-ampasua-mashinji-baada-ya-kupata-kura-2/

No comments:

Post a Comment