Thursday, July 9, 2020

Diamond na Zari Warejeleana? Amzawidi gari la kifahari

I have already reached out to Zari,” Diamond Platnumz responds to ...

Uhusiano kati ya Diamond Platnamz na Zari Hassan umeonekana kufufuka kwa muda sasa

Hili limebainika zaidi baada ya zari kujitokeza na kujishaua kwa gari la kifahari alilozawadiwa na Mondi

Aliye na macho haambiwi tazama, hii ndiyo hali halisi kuhusu uhusiano kati ya msanii maarufu wa Bongo Diamond Platnamz na mpenzi wa zamani Zari Hassan.

Licha ya wawili hao kuonyeshana visogo miaka michace iliyopita, sasa ni wazi kuwa wananyemeleana, na Zari hayuko tayari tena kuficha.

Hili lilikuwa wazi pale Zari alipoiwasha mitandao haswa Instagram kwa kuipakia gari aina ya Bentley aliyoashiria kuzawadiwa na Diamond Platnumz.

‘’Thank you T’s dad (Princess Tiffah) for the top-up,’’ Zari aliaindika chini ya picha hiyo.

View this post on Instagram

Zari Hassan gifted new Bentley by Diamond Platnumz.. 😍

A post shared by Urban News (@urbannews254) on

Gari hilo lilikuwa limepambwa na maua mekundu, nani asiyejua kuwa hiyo ni rangi ya kuashiria mapenzi?

Jarida la Bongo Leo lilizama kukutafutia bei kamili ya gari hilo na likathibitisha kuwa unahitaji Tsh 780,000,000 kulinunua, hivyo ndivyo Diamond alivyogharamika kumuonyeha Zari kuwa angali anamthamini.

View this post on Instagram

❤🌹 @mama_dangote 🌹❤

A post shared by SIMBA..!🦁 (@diamondplatnumz) on

Si hilo tu, wiki chache tu kabla, Mondi alimtumia mwanawe, Tiffah kifurushi cha vyombo vya jikoni. Zari alionyesha shukrani akifanya video na kuchapisha mtandaoni kifurushi hicho.

View this post on Instagram

Someone is so Happy Today 😋😊🥰 @Princess_Tiffah ❣❤

A post shared by SIMBA..!🦁 (@diamondplatnumz) on

Licha ya Diamond kufanya hayo yote kumkwachua tena Zari, mrembo huyu amesisitiza kuwa hayuko tayari kumrejelea Mondi, kwa upande wake alieleza kuwa Diamond amefunguka macho na kuona makosa yake na yuko tayari kujihusisha katika maisha ya wanawe.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/07/09/diamond-na-zari-warejeleana-amzawidi-gari-la-kifahari/

No comments:

Post a Comment