Mahabara ya hospitali ya Langata ilifungwa moja kwa moja na maafisa wa bodi ya kusimamia maabara nchini (KMLTTB)
Msako huo ulifanyika Jumatano, Julai 8 baada ya fununu kuvuja kuhusu kufanyika vipimo feki vya virusi vya corona hospitalini humo
Maafisa hao walipata habari kuwa hospitali hiyo ilikuwa ikilipisha Tsh 115,500 kwa vipimi hivyo
Maabara ya hospitali ya Langata itasalia kuwa mahame baada ya kupewa amri ya kufunga kufuatia vipimo na matokeo feki ya covid19 ambavyo vimedaiwa kufanyika hospitalini humo.
Kulingana na bodi ya kusimamia maabara nchini KMLTTB, maabara hayo yamekuwa yakiwalipisha wananchi kima cha TSh 115,500 kwa vipimo hivyo na baadaye kusafirisha sampo hizo kwa kutumia ambulensi hadi KEMRI kwa majaribio.
Bodi hiyo ilieleza kuwa maabara ya hospitali hiyo haina vifaa vya kutumika katika vipimo vya virusi vya corona na hivyo haifai kabisa kujihusisha na vipimo hivyo.
‘’Kilichotufanya kuyafunga maabara haya ni kuwa wanawahadaa wananchi kuwa wanafanya vipimo vya corona wakati siyo wanayofanya,’’ Alisema afisa mkuu mtendaji wa bodi hiyo Patrick Kibet.
‘’ Pia tumejaribu kuangalia kama kuna maelewano kati ya KEMRI na maabara haya kuhusu kufanyika vipimo na tumepata waraka ambao sasa utafanyiwa uchunguzi zaidi,’’ aliongezea.
Kulingana na kiongozi huyo, vifaa vinavyotumika katika maabara hiyo ni vile ambavyo vimeharibika
Polisi sasa wameanza uchunguzi zaidi kuhusu suala hilo nzima.
source http://www.bongoleo.com/2020/07/09/mahabara-ya-hospitali-maarufu-kenya-yafungwa-kwa-kufanya-vipimo-feki-vya-covid19/
No comments:
Post a Comment