Thursday, July 9, 2020

Sakata La Shilole Na Uchebe : Mshenga Afunguka A-Z

ImageIkiwa yamepita masaa kadhaa tangu msanii wa muziki wa kizazi kipya Zuena Mohammed (Shilole) kutangaza kuvunja ndoa yake na aliyekuwa mume wake Ashrafu Sadick (Uchebe) kutokana na vitendo vya ukatili.

Mshenga aliyefungisha ndoa ya wawili hao Alawiy Alhaddad amesema ameshawahi kumuonya aliyekuwa mume wa Shilole mara kadhaa juu ya vitendo vya kumpiga mwanamke huyo lakini hakuwa mtu anayesikiliza.

“Binafsi nimeikemea ndoa hii hasa masuala ya Shilole kupigwa, sio mara moja nimejaribu kumuonya atumie hekima, busara ili kufikia muafaka, asitumie mabavu kumpiga yule binti, Uchebe hajawahi kuniletea kesi kwamba Shilole amemfanyia ubaya” amesema Alawiy Alhaddah akihojiwa na East Africa Radio.

Mapema jana Julai 8, 2020 mwanamuzki Shilole aliweka uumbe kwenye ukurasa wake wa instagram akimlaumu uchube kuwa alikuwa akimpiga mara kwa mara nankutangaza kuvunja ndoa hiyo iliyodumu kwa takribani miaka miwili.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/07/09/sakata-la-shilole-na-uchebe-mshenga-afunguka-a-z/

No comments:

Post a Comment