Thursday, July 23, 2020

CCM yamlilia Rais Mstaafu Mkapa, imesema imepata pigo kubwa

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema kimepokea kwa masikitiko na huzuni kubwa taarifa ya kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wao na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin William Mkapa.

Rais Mstaafu Mkapa amefariki usiku wa kuamkia leo akiwa amelazwa hospitali jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole, ameeleza kuwa Rais John Magufuli amewataka Watanzania kuwa watulivu na watahimilivu  baada ya kutokea kifo  cha mpendwa wao mzee Benjamin Mkapa.

“Kwa masikitiko makubwa tumepata msiba mkubwa , Mzee wetu Benjamini William Mkapa, Mwenyekiti wa CCM Mstaafu na Rais Mstaafu  wa awamu ya tatu amefariki dunia, amefariki dunia katika hospitali ya jijini Dar es Salaam ambapo alikuwa amelazwa. Niwaombea Watanzania mlipokee hili, tumepata msiba mkubwa  na tunaendelea kumuombea mzee wetu,” amesema mwenyekiti wa CCM na Rais John Magufuli.

Taarifa nyingine kuhusiana na msiba huo mkubwa zitatolewa kwa baadaye.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/24/ccm-yamlilia-rais-mstaafu-mkapa-imesema-imepata-pigo-kubwa/

No comments:

Post a Comment