Thursday, July 23, 2020

Dk.Nchemba, Ummy, Dk. Kigwangalla, Bashe, Nape, Makamba na Mo wamlilia Mpaka

Viongozi, wanasiasa na wafanyabiashara wamesikitishwa na kifo cha Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamini Mkapa aliyeafariki usiku wa kuamkia leo akiwa amelazwa hospitali jijini Dar es Salaam.

Wadau hao waliandika ujumbe kwa tofauti kupitia ukurasa zao za kijamii huku wakionyesha masikitiko yao kwa kifo cha Rais mstaafu, Benjamini Mkapa.

Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Mwigulu Nchemba, amesema amepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha Rais Mstaafu Mkapa “Tumepoteza moja ya nguvu imara katika taifa letu, pumzika kwa amani baba,”.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema ni majozi makubwa kwa Tanzania na tumuombee Rais Mstaafu Mkapa apumzike kwa amani “Natoa pole kwa mke wa marehemu Mama Anna Mkapa, watoto, familia, jamaa, marafiki na Watanzania wote. Bwana ametoa, bwana ametwaa,”.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamis Kigwangalla amesema amepokea taarifa za msiba wa mzee Mkapa kwa masikitiko makubwa sana. “Natuma salamu zangu za pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na watanzania wenzangu wote. pumzika kwa amani baba yetu,”.

Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe aliandika ujumbe huu katika ukurasa wake wa twitter “Nimepokea kwa mshtuko taraifa ya msiba wa mzee wetu Benjamini William Mkapa Rais wa awamu ya tatu huu ni msiba mzito kwa taifa letu kama ambavyo mh Rais John Magufuli alivyosema wakati akitangaza,”.

Aliongezea kuwa “Mzee mkapa ametuachia hazina ya kutosha katika maandishi yake, mzee mkapa ameondoka akiwa bado ni PanAfricanist,”

Aliyekuwa mbunge wa Bumbuli, January Makamba, ameandika ujumbe huu “Bado ni vigumu kukubali mzee Mkapa hatunaye tena “Pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wote. Ni msiba mzito kwa taifa letu mwenyezi Mungu amlaze Mzee wetu pema peponi,”

Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Mtama, Nape Nnauye aliandika ujumbea huu ” What a loss!!! Nakumbuka upendo wake, malezi na busara zako nikiwa Mkuu wa Wilaya Masasi! Aaaah, mwamba mwenye sifa  halisi za kusini what loss!! Pumzika baba,”.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila amesema mzee Mkpa alichukua nafasi kubwa kukuza na kuimarisha uchumi wa Tanzania.

Mfanyabiashara Mohammed Dewji maarufu kwa jina la MO amesema bado ni ngumu kukubali kwamba mzee Mkapa kaondoka.

“Pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na watanzania kwa ujumla kwa msina huu mzito. Mwenyezi Mungu aipumzishe roho yake mahali peponi,”.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/07/24/dk-nchemba-ummy-dk-kigwangalla-bashe-nape-makamba-na-mo-wamlilia-mpaka/

No comments:

Post a Comment