Thursday, July 23, 2020

Rais Magufuli atangaza siku saba za maombolezo kitaifa kwa msiba wa Rais Mstaafu Mkapa

Rais John Magufuli ametangaza siku saba za maombolezo ya kitaifa kuanzia leo kutokana na kifo cha Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamini Mkapa, kilichotokea usiku wa kuamkia leo jijini Dar es Salaam.

Rais Magufuli amesema katika kipindi cha maombolezo bendera zote zipeperushwe nusu mlingoti.

Aidha, Rais amewaomba Watanzania wote kuendelea kuwa watulivu, wastahimilivu na wamoja katika kipindi hiki kigumu cha majozi ya kuondokewa na mpendwa wao Rais Mstaafu Mkapa.

Taarifa zingine kuhusunia na msiba huo mkubwa kwa taifa zitatolewa baadaye.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/24/rais-magufuli-atangaza-siku-saba-za-maombolezo-kitaifa-kwa-msiba-wa-rais-mstaafu-mkapa/

No comments:

Post a Comment