Tuesday, July 21, 2020

Mgombea alivyoibua kicheko kwa wapiga kura baada ya kuomba kura kwa kichina

Katika hali isiyo ya kawaida mgombea mmoja katika jimbo la Kawe jijini Dar es Salaam ameongea lugha ya kichina wakati akiomba kupigiwa kura kwa ajili ya kuwania ubunge katika jimbo hilo.

Jimbo la Kawe lilikuwa na wagombea 170 ambao leo kila mmoja alikuwa akijinadi kwa kuweka sera zao ili waweze kuchaguliwa katika uchaguzi huo wa kura za maoni.

Zamu yake ilipofika aliingia katika ukimbi wa mkutanao kwa mbwembwe akiwa ni mwenye namba 75 alianza hivi “Wakubwa zangu shikamooni,  Rais wa kwanza wa awamu..awamu..rais wakwanza wa China anaseema….,”
Mgombea huyo ndipo alipoanza kuongea kwa kichana na kusababisha watu kuangua kicheko katika mkutano huo.

Baada ya kuongea kichina alitafsiri kwa kiswahi kwa kusema kuwa wajibu wake ni kuwajibika kwa maneno, kwa vitendo na kwa sera ili waeweze kutatua kero za wananchi.

“Kwa kutumia ilani ya Chama cha Mapinduzi nitatekeleza kwa vitendo, maneno kama avyosema mwasisi wetu,”
Baada ya kueleza hayo aliomba wampigie kura ambapo alimalizia kutamka maneno hayo kwa kutumia lugha ya kichina huku wakicheka na kumshangilia.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/21/mgombea-alivyoibua-kicheko-kwa-wapiga-kura-baada-ya-kuomba-kura-kwa-kichina/

No comments:

Post a Comment