Tuesday, July 21, 2020

Mwanamke Amuiba Mtoto wa Rafiki Kumfurahisha Mumewe, Ajifanya Amejifungua

Voi woman in distress as friend she hosted goes missing with her baby

Moureen hakurudi tena na mwanawe, Rhoda akilazimika kupiga ripoti kwa polisi. Picha; Hisani

Maureen alimtembelea rafikiye Rhoda Nyanjama baada ya kupata taarifa kuwa alijifungua

Walikuwa na rafiki huyo, asubuhi Moureen alitoka na mtoto kuenda dukani

Hakurudi tena, Rhoda akilazimika kupiga ripoti kwa polisi

Mwanamke mmoja mkazi wa Voi ameuomba umma kumsaidia kumpata mwanawe mpendwa wa miezi mitatu aliyeibwa na rafiki wa karibu.

Kulingana na kisa hicho kilichofanyika Taita Taveta, Rhoda Nyanjama alieleza kuwa rafikiye, Moureen ambaye anatambulika na wengi kama Msichana wa Nzomo alitoroka na mwanawe mchanga asubuhi akieleza kuwa walikuwa wanaenda dukani Jumatano, Julai 16 lakini hawakurudi tena.

Alieleza kuwa Moureen alikuwa rafiki yake na walijuana Mombasa walikokuwa wakifanya biashara rejareja.

‘’ Sikufikiri alikuwa na nia ya kumuiba mtoto wangu, nilimsuburi arudi lakini wapi.’’ Njanjama alisema.

Kisa hicho kiliripotiwa katika kituo cha polisi cha Maungu na polisi wameanza uchunguzi.

Shirtless Man Riding Atop Police Car in CBD Lights Up The Internet ...

Polisi sasa wameanzisha msako mkali dhidi yake na mshukiwa. Picha: Hisani.

Katika uchunguzi huo, msichana mwengine aliyekamatwa kama mshukiwa alieleza kuwa Msichana wa Nzomo alilala kwake usiku kabla kufika kwa Rhoda na alimueleza kuhusu jinsi alivyokuwa akitamani kupata mtoto na jinsi alivyofeki kuwa ana ujauzito na kuwa alihitajika kurudi nyumbani akiwa na mtoto.

Polisi sasa wameanzisha msako mkali dhidi yake na mshukiwa huyo huku wakimtaka kila aliye na ripoti kumhusu kuwasilisha katka kituo chochote.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/21/mwanamke-amuiba-mtoto-wa-rafiki-kumfurahisha-mumewe-ajifanya-amejifungua/

No comments:

Post a Comment