Baada ya sakata la wanafunzi wa vyuo mbalimbali nchini kulalamika kupunguziwa pesa za kujikimu na bodi ya mikopo kuliko ilivyo kawaida ya pesa wanapewa kila mwezi kama sehemu ya kujikimu wanapokuwa masomoni.
Leo Juali 23, 2020 bodi ya mikopo nchini imetoa ufafanuzi juu ya hali ilivyo kwa wanafunzi walilalamika kupunguziwa pesa za kujikimu kwenye kipindi cha miezi kadha ailiyosalia cha kukaa chuoni.
“Malengo ya fedha hizi ni kunufaisha wanafunzi ili kuongeza wasomi wengi nchini, pesa zinalipwa kulingana na muongozo na ratiba ya chuo husika, kama chuo kikisema utakaa chuo kwa siku ishirini utapatiwa pesa ya siku ishirini bila upungufu wowote, lakini kinachotokea hapa ni mwanafunzi anataka alipwe hadi muda ambao yuko likizo”amesema mkuu wa kitengo cha Mwasiliano Omega Ngole.
source http://www.bongoleo.com/2020/07/23/bodi-ya-mikopo-yatoa-ufafanuzi-wanafunzi-kupunguziwa-fedha/
No comments:
Post a Comment