Thursday, July 9, 2020

Wema Afunguka “Diamond Ni Mpigaji Sana”

Diamond Platnumz Confirms He'll Be Walking Down the Aisle With SepetuIkiwa ni takribani siku moja tangu msanii wa muziki wa kizazj kipya Zuena Mohammed (Shilole) kuweka wazi kuwa amekuwa akipingwa mara kwa mara na aliyekuwa mume wake Ashrafu Sadick.

Muigizaji Wema Sepetu ameweka wazi kuwa hata yeye alikuwa anapigwa na aliyekuwa mpenzi wake msanii mwenzie Naseeb Abdul (Diamond) lakini alikuwa akifurahia na hakuripoti popote juu ya ukatili huo.

Akinukuliwa na gazeti la Uwazi Wema amesema Diamond ameshawahi kumpiga mara nyingi na hata ndugu zake walisha wahi kutaka kwenda kuripoti juu ya tukio hilo.

“Ninachokumbuka sana ni kipigo chake. Aisee kilikuwa hatari lakini nilikuwa napenda kupigwa naye kwa sababu alikua akinipiga ananibembeleza sana basi na enjoy.” Amenukuliwa Wema.

Wema pia amekumbushia moja kati ya vipigo alivyo amewahi kupata toka kwa mwana muziki huyo ambaye wameachana sasa.

“Kuna siku Nasib alionaga meseji imeingia kwangu akawa na wasiwasi nayo. Akanipiga kibao kikali kwenye shavu, halafu ndugu zangu wakajua. Hata nyinyi mlitoa kwenye gazeti. Lakini niliwaambia mimi napenda kupigwa naye hivyo waniache. Mimi nikipenda ndivyo nilivyo” Ameongeza.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/09/wema-afunguka-diamond-ni-mpigaji-sana/

No comments:

Post a Comment