Thursday, July 9, 2020

Mfanyakazi wa ndani aua kikatili watoto wawili kwa kuwakata kwa panga na yeye kuuliwa na wananchi

Mfanyakazi wa ndani, Yasin Abdalah, (35) ameuwa watoto wawili kikatili kwa kuwakata mapanga na kisha na yeye akauliwa na wananchi.

Watoto waliouliwa ni Rehema Azizi mwenye umri wa miaka mitano ambaye anasoma shule ya awali ya Kazoka Abubakari Azizi mwenye umri wa miaka sita anasoma darasa la kwanza katika shule ya msingi ya Kazoka.

Baada ya kufanya kwa tukio hilo alikamatwa na kuwekwa kwenye serikali za mtaa ambapo alitoroka na wananchi wenye hasira kali wakamkimbiza na kumuua.

Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani, Mwakyo Nyigesa, amesema tukio hilo limetokea jana saa 1 usiku katika kitongoji cha kivungwi Kazoka kata ya Vingwaza Wilaya ya Bagamoyo.

Amesema  kijana huyo alikuwa akifanya kazi kwa Wema Sinzia aliwaua wato

Kamanda alisema kijana huyo kabla ya kuuliwa alikamatwa na kuwekwa kwenye kituo cha ofisi ya Kitongoji cha Kazoka na kufungiwa katika ofisi hiyo.

Alisema kijana huyo alivunja mlango wa ofisi hiyo na kutoroka ndipo wananchi walivyokwenda kumkamata na kumuua.

Kamanda alitoa rai kwa wananchi kuhakikisha kuwa wanapomkamata mtuhumiwa wasijichukuliea sheria mkononi.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/09/mfanyakazi-wa-ndani-aua-kikatili-watoto-wawili-kwa-kuwakata-kwa-panga-na-yeye-kuuliwa-na-wananchi/

No comments:

Post a Comment