Thursday, July 23, 2020

Watumishi tisa wa Takukuru wamesemamishwa kazi sakata la Magufuli

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Bregedia Jenerali, John Mbung’o amewasimamisha kazi watumishi tisa.

Watumishi hao ambao wamesimamishwa kazi wamehusika katika ujenzi na usimamizi wa majengo saba ya Takukuru.

Majengo hayo ambazo yapo Chamwino, Mpwapwa, Ngorongoro, Manyoni, Masasi, Namtumbo na Ruangwa.

Mbung’o amesema imeundwa Tume yenye watu wanne kutoka nje ya Takukuru kwa ajili ya kufautailia kama kuna ubadhirifu uliofanyika katika majengo yaliyojengwa.

Jana Rais John Magufuli, wakati akizindua jengo la Chamwino alisema anayazindua huku moyo wake ukimuua kwa kuwa Takukuru wamepigwa katika ujenzi huo.

Magufuli amesema jengo kama hilo halina uhalisia wa thani ya Sh milioni 134 kwa kuwa yeye alishwahi kujenga nyumba ya aina hiyo kwa Sh milioni 40.

Rais aliagiza kufanyika kwa uchunguzi wa ujenzi wa nyumba hizo kutokana na gharama zake kuwa kubwa huku akiwashaanga Takukuru iweje na wao wapigwe fedha katika nyumba hizo.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/23/watumishi-tisa-wa-takukuru-wamesemamishwa-kazi-sakata-la-magufuli/

No comments:

Post a Comment