Thursday, July 23, 2020

Mmiliki wa Shule Ageuza Darasa Karakana ya kuunda Viti Kufuatia Janga la Corona

Mombasa: Private school owner turns classrooms into workshops as COVID-19 bites

Shadrack Atik, mmiliki wa shule ya New Shamy ameelza kuwa alichukua hatua hiyo kuhakikisha haifilisiki

Shule hiyo ilikuwa na idadi ya wanafunzi 350 na walimu 15

Mmiliki mmoja wa shule ya kibinafsi mjini Mombasa amelazimika kuwa mbunifu baada ya shule kufungwa tangu virusi vya corona viliporipotiwa nchini.

Shadrack atik, mmiliki wa shule ya New Shamy aliamua kuygeuza madarasa yake kuwa karakana ya kuunda viti, vitandana kama njia ya kujikimu kimaisha.

Atik alieleza kuwa ilikuwa muhimu kuhakikisha kuwa shule hiyo haianguki licha ya kufungwa miezi mine iliyopita na hivyo akatafuta njia mbadala ya kuiendeleza kwa kulipa kodi.

Kuendelea kumiliki jengo hilo ndiyo muhimu zaidi. Kwa hivyo kutokana na biashara hii mpya, tutaweza kupata pesa za kulipa kodi.  Pia tutatumi pesa hizo kuwalipa walipa walimu kitu kidogo ili kuwasaidia wakati huu mgumu,’’ alisema.

Mombasa: Private school owner turns classrooms into workshops as COVID-19 bites

Shule hiyo ya New Shamy ilikuwa na idadi ya wanafunzi 350 na walimu 15 kabla kufungwa kufuatia mlipuko wa virusi vya corona, Atik akisisitiza kuwa hataweza kupata idadi hiyo tena 2021 shule zinapofunulwa tena.

Aidha alieleza kuwa ameweza kuwaajiri walimu wanne katika karakana yake ili kupata nji ya kujikimu.

‘’ Sijaweza kuwalipa walimu haswa baada ya shule kufungwa, hata hivyo, katika bishara yangu mpya, nimewaajiri wanne maana walikuwa na ujuzi wa kuunda viti,’’ aliongezea.

Haya yanajiri siku chachetu baada ya jarida la Bongo Leo kuripoti kuhusu kisa cha mmiliki mwengine wa sule aliyelazimika kuigeuza uwanja wa shule kuwa shamba la mboga.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/23/mmiliki-wa-shule-ageuza-darasa-karakana-ya-kuunda-viti-kufuatia-janga-la-corona/

No comments:

Post a Comment