Thursday, July 9, 2020

Wajanja hatulindi demu huwa tunafanya haya upo?

 

Habari ya muda huu msomaji wangu karibu katika ukurasa wetu wa mahusiano tuweze kujifunza mambo mbalimbali.

Leo nipo na wewe mwanzo mwisho na mada yetu ni konki mwanamke hawindwi jamani mpe Uhuru wake.

Mpe Mpenzi wako sababu ya yeye kujilinda akiwa mwenyewe hata kama haupo…Usitumie nguvu na ubabe kumlinda kama hana sababu ya yeye kujilinda mwenyewe.

Mpende na ajue anapendwa ili asiwe na sababu ya kuuchakachua upendo unaompa maana unamtosha kumlinda dhidi ya maupendo feki ya mtaani.

Sasa wewe badala ya ku-invest muda wako kumpa upendo wa kutosha, umejigeuza Alarm, kwamba unaweza kumlinda asiibiwe au asikusaliti jamani wanaume mnafeli wapi.

Unapoteza muda kumfuatilia anaenda wapi, na nani, na kwa nini hajaaga,unamfuatilia nani kamtumia meseji na nani anaongea nae kwa simu mpaka unaenda kuprint statement kwenye mtandao anaotumia kuwa anaeasiliana na nani.

Unapoteza muda wako kama hujawahi kumiliki hata shina la mgomba utawezaje kumiliki mtu??? Mwanamke hawindwi wekeza upendo katika penzi utafurahi mwenyewe. Kuku wako mwenyewe manati ya nini?

Mpenzi halindwi kama alarm, watu watamuiba  mchana kweule mpe sababu za kujiona anapendwa ili ajilinde mwenyewe.

Kumlinda Mpenzi ni sawa na kulinda Bahari, wewe unalinda Coco Beach wenzio wanavua samaki Bagamoyo.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/09/wajanja-hatulindi-demu-huwa-tunafanya-haya-upo/

No comments:

Post a Comment