Maggie alipigwa na mshangao kugundua kuwa alikuwa akitarajia mapacha watatu
Alipata mshangao mkubwa zaidi tena baada ya kupatikana na virusi vya corona akiwa una uja uzito wa miezi saba
Aliingiwa na wasiwasi mkubwa kuhusu hali ya afya ya wanawe
Mwezi mmoja kabla ya kujifungua alifanyiwa vipomo na kupataikana alipona kutokana na virusi hivyo
Mwanamke mmoja raia wa Amerika amepata sababu ya kumshukuru Mungu maradufu baada ya kujifungua mapacha watatu katika hali isiyo ya kawaida.
Maggie ambaye alijifungua mapacha hao aliugua ugonjwa wa corona miezi michache tu kabla ya kujifungua wanawe suala ambalo lilimtia wasiwasi mkubwa.
‘’Wiki moja tu baada ya kupataa ujauzito, nilikuwa nikihisi madadiliko kadhaa. Nadhani ilikuwa hivyo kwa maana nilikuwa na mapacha. Dalili zagu zilikuwa maradufu,’’ Maggie alilimbia jarida la Goodmorning America.
Kulingana naye, hakuamini kuwa angeweza kujifungua mapacha hao haswa kutokana na hali yake ya kiafya iliyozidi kuzoroteka.
Habari kuhusu kuugua kwake iligunduliwa baada ya kulazwa hospitalini akiwa na ujauzito wa miezi saba, hali yake ikihitaji uangalizi wa karibu.
Maggie alijaliwa, mwezi mmoja kabla ya kujifungua, alipimwa tena baada ya matibabu kadhaa na kubainika kuwa alipona kutokana na virusi hivyo.
Wiki chache baadaye, alijifungua mapacha watatu, wawili wa kiume na msichana, furaha iliyoje?
source http://www.bongoleo.com/2020/07/10/mama-aliyeugua-covid19-ajifungua-mapacha-watatu/
No comments:
Post a Comment