Wednesday, July 22, 2020

Heche: Madagascar wanaomba msaada katika Corona wakati tulituma ndege kuchukua dawa

Aliyekuwa Mbunge wa Tarime Vijini (Chadema), John Heche, amehoji kitendo cha Madagascar kuomba msaada katika kukabiliana na ugongwa wa Corona licha ya kutangaza wana dawa ya kutibu.

“Si nakumbuka Kabudi alienda kuchukua dawa hapa.. tulituma ndege kuchukua dawa alafu wao wanaomba msaada…” aliandika Heche katika ukurasa wake wa twitter.

Madagascar imeanza kuhaha kutafuta misaada toka Mashirika na Taasisi za Afya za Kimataifa kukabiliana na kuenea kwa kasi kwa wagonjwa wa Corona katika wiki mbili.

Wagonjwa ambao wanaumwa Corona Madagascar wamefikia 8,557 waliopona  4,662 na vifo ni 72.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/23/heche-madagascar-wanaomba-msaada-katika-corona-wakati-tulituma-ndege-kuchukua-dawa/

No comments:

Post a Comment