Wednesday, July 22, 2020

Dondoo za leo: Polepole aeleza hatma ya wagombea waliofungana kura za maoni, Waliogombea kukatwa mshahara na Heche ahoji Madagascar kuomba msaada kwenye Corona

 

Habari ya asubuhi mdau wa Opera News ni siku nyingine ya Alhamisi Julai 23, 2020, matumaini yetu upo salama na karibu katika ujenzi wa taifa.

Tunakukaribusha katika dawati letu la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazopamba asubuhi ya leo.

Habari hizo ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole, ameeleza hatma ya wagombea waliofungana kwenye kura za maoni je unajua ni kipi alichokieleza?, Serikali imeagiza waliogombea kukatwa mishahara yao na Heche ahoji Madagascar kutaka msada kwenye ugonjwa wa Corona kulikoni?

Karibu msomaji wetu;

POLEPOLE AELEZA HATMA YA WAGOMBEA WALIOFUNGANA KWENYE KURA ZA MAONI

Katibu Mkuu Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey polepole amesema waliofungana katika kura za maoni wasiwe na hofu wao wataendelea na mchakato wao wa vikao kuweka mapendekezo.

Polepole ametoa kauli hiyo baada ya watia nia kufungana matokeo  katika kura za uchaguzi za wagombea katika majimbo.

“Limekuwepo swali katika kura hizi za maoni kuwa kuna maeneo mengine ambapo wagombea wamefungana kwa idadi ya kura mfano Mwibara , Sengerema sasa hiii isiwaletee hofu,”amesema Polepole.

Soma zaidi

HAZINA YAAGIZA WALIOTIA NIA  KUTOLIPWA MSHAHARA

OFISI ya Msajili wa Hazina, imewataka wakurugenzi wote wa Halmashauri na Taasisi zote za serikali kutowalipa mshahara wa Julai watumishi wake wote waliochukua fomu ya kugombea nafasi ya uongozi wa kisiasa kupitia vyama vya siasa.

Kwa mujibu wa barua iliyoandikwa Julai 21, mwaka huu na Msajili wa Hazina, Neema Msonda ambayo imesambaswa katika taasisi hizo za serikali, imewataka pia wakurugenzi na wakuu wa taasisi hizo kuandaa na kuwasilisha katika ofisi ya Msajili wa Hazina, taarifa ya utekelezaji wa maelekezo hayo kabla au ifikapo Julai 25.

Soma zaidi

HECHE: MADAGASCAR WANAOMBA MSAADA KATIKA CORONA WAKATI TULITUMA NDEGE KUCHUKUA DAWA

Aliyekuwa Mbunge wa Tarime Vijini (Chadema), John Heche, amehoji kitendo cha Madagascar kuomba msaada katika kukabiliana na ugongwa wa Corona licha ya kutangaza wana dawa ya kutibu.

“Si nakumbuka Kabudi alienda kuchukua dawa hapa.. tulituma ndege kuchukua dawa alafu wao wanaomba msaada…” aliandika Heche katika ukurasa wake wa twitter.

Soma zaidi

 



source http://www.bongoleo.com/2020/07/23/dondoo-za-leo-polepole-aeleza-hatima-ya-wagombea-waliofungana-kura-za-maoni-waliogombea-kukatwa-mshahara-na-heche-ahoji-madagascar-kuomba-msaada-kwenye-corona/

No comments:

Post a Comment