Tuesday, July 21, 2020

Pacha wa Waziri wa Madini ameibuka mshindi kura za maoni

 

Mgombea Ubunge, Kulwa Biteko ameibuka kidedea katika uchaguzi wa kura za maoni katika jimbo la Busanda kwa kupata kura 665.

Kulwa ambaye ni pacha wa  Waziri wa Madini, Doto Biteko.

Katika uchaguzi huo aliyeshika nafasi ya pili ni Laulencia Bukwimba 94 na watatu ni Abdala Hussein 20.

Waziri Doto Biteko

Kwa upande wa Doto Biteko ambaye alijitokeza kutia nia jimbo la Bukombe ameibuka na ushindi kwa kupata kura 555.

Mshindi  wa pili ni Mihayo Paul alipata kura mbili na Mkama Mashinagu ambaye aliambulia sifuri.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/22/pacha-wa-waziri-wa-madini-ameibuka-mshindi-kura-za-maoni/

No comments:

Post a Comment