Esma hakuona lolote la maana katika kutembea kwa mtoto huyo. Picha: HIsani
Esma Platnamz ambaye pia ni dadake msanii Diamond alijipata kwenye sinia ya pilipili baada ya kuchekelea video ya mwanawe Tanasha Donna, Nassseb JNr akitembea kwa mara ya kwanza.
Ilikuwa siku ya kuzaliwa kwa mamake Diamond na hivyo alikuwa amejiandaa kwa sherehe, sadfa iliyototokea ni kuwa siiku hiyo hiyo ndiyo mwanawe Tanasha akaweza kutembea kwa mara ya kwanza kabisa.
Mamake Diamond ni kati ya watu waliojitokeza kumfurahia mtoto huyo, akishangaa ni kwanini mtoto huyu alisubiri hadi siku yake akatembea.
‘’Kweli leo nimeonyeshwa surprise na Bwana Naseeb tom kaka kasikia leo mkewe kazaliwa na yy katembea kweli Bwana Naseeb ananipenda anataka aje afurahi na mm Mkewe,’’Aliandika.
Esma kwa upande wake hakuona lolote la maana katika kutembea kwa mtoto huyo na hivyo akachapisha alama ya kicheko tu.
Baadhi ya mashabiki waliokuwa na hisia kuwa Esma alifanya kitu kibaya hawakuchelewa kujimwaya mitandaoni kumrundia mabiwi ya matusi kwa kumkosea adabu Tanasha Donna.
Licha ya wengi kusubiri kusikia kauli ya Esma baada ya kushambulia, kama kawaida, mwanadada amesalia kimya bila kutamka lolote wala kumjibu yeyote.
Baadhi sasa wanadai kuwa lengo la kuchapisha video ya mtoto huyo akitembea lilikuwa ni kukipa umaarufu kibao cha Abamako.
Ikimbukwe kuwa Mondi Na Tanasha Donna walikosana na kutemana mapema Februari 2020, uvumu ukienea kuwa Esma ni kati ya wahusika wakuu waliochangia mvutano kati ya wawili hao, swala ambalo hadi sasa Esma hajakiri wala kukana.
source http://www.bongoleo.com/2020/07/08/dadake-diamond-platnumz-ajipata-pabaya-kwa-kumchekelea-mwanawe-tanasha-donna/
No comments:
Post a Comment