Sunday, August 9, 2020

Usije kumnyima mpenzi wako uchi kisa amekuuzi upo?

 

Habari ya muda huu msomaji wangu. Karibu katika ukurasa wetu wa mahusiano uweze kujifunza mambo mbalimbali.

Kuna baadhi ya vitu hutokea katika maisha hasa kwa wale wanaoishi pamoja na wapenzi wao na hauwezi kuzuia yasitokee.

Changamoto za hapa na pale lazima zitokee hakuna ambaye ni mkamilifu kwa mwenzake, hivyo tunatakiwa kuchukuliana madhaifu ili maisha yaende.

Inapotokea mpenzi wako amekukosea huna sababu ya kumuadhibi kwa kulala mzungu wanne.

Sijaelewa ukubwa wa kosa alilokukosea lakini suluhu ni kuitafuta mapema usisubiri yakatokea madhara zaidi.

Jitahidi kumuambia mpenzi wako makosa yake usiweke visasi moyoni maana haitasaidia katika kujenga penzi lenu.

Wapo wengine wakishaona waume zao wamewakosea wanalala mzungu wa nne hii ni kuongeza ukubwa wa tatizo na kumfanya mwanaume azidi kutoka nje.

Ifahamike kuwa, hata kama ulimfuma na mwanamke sasa utamfanya penzi lihamie kwa mke mweza huku wewe ukiendelea kuumia.

Nani kakuambia ukilala mzungu wa nne unamkomesha mwanaume wako kwa jambo alilokuuzi hapa ni kumpa mpenyo wa kuendelea kuchepuka.

Jitahidi kuwa mbunifu pale mpenzi wako anapokuuzi na umjulishe ukweli wa kosa hilo mpenzi wako ili asilirudie.

Kama kweli anakupenda atakusikiliza na kama hataki kujirekebisha jua hakupendi maana mwanaume anayekupenda hawezi kukubali kukuumiza kila wakati.

Anapokuwa anahitaji mchezo wa chumbani mpatie bila kusita lakini unaweza kuitumia nafasi hiyo kabla ya kuaza kwa tendo la ndoa kuombana msamaha.

Ni vizuri mnapokuwa kwenye sita kwa sita wote mkawa na furaha sio mmoja ana hasira na mwenzake inakuwa haipendezi.

 

Mkamate vizuri mpenzi wako mpe vitu hadimu hadi abaki na maswali ya kujiuliza achana na huo mchezo wa kulala mzungu wa nne haitakusaidia kujenga mahusiano yenu.

Wakati mwingine utaona kama ni vigumu kunielewa ila ukweli ndio huo usikubali kutoa nafasi ya mume wako kwenda kwa mchepuko hata kama amekuudhi suluhu haipo kulala mzungu wa nne.

Asikuambie mtu safari ya kupanda mlima Kilimanjaro ina raha yake hasa wote mkiwa kwenye furaha na ushindi ukapatikana kwa kila mmoja. Ina raha yake.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/08/09/usije-kumnyima-mpenzi-wako-uchi-kisa-amekuuzi-upo/

No comments:

Post a Comment