Thursday, August 13, 2020

Ofisi ya Chadema yalipuliwa kwa Petroli na kuteketea

Ofisi ya chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kanda ya Kaskazini imechomwa moto na kuteketea usiku wa kuamkia leo mkoani Arusha.

Kwa mujibu wa taarifa ambayo ameitoa Aliyekuwa mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee kupitia ukurasa wake wa twitter.

“Ofisi yetu ya @Chademakaskazini imechomwa moto na kuteketea yote usiku wa kuamkia leo,” aliandika Mdee.

“Ikumbukwe mgombea urais @ TunduALissu ameanza  jana ziara ya kutafuta wadhamini kanda ya Kaskazini!! Tunawaambia @ccm _Tanzania…. Vitisho vya kishamba

Sasabaaaaaaaaaaaasi,” aliandika Mdee.

Habari za awali inadaiwa kuwa jengo hilo limemwagiwa petroli madirisha yote na moto uliwashwa  mlango wa mbele mapokezi.



source http://www.bongoleo.com/2020/08/14/ofisi-ya-chadema-yalipuliwa-kwa-petroli-na-kuteketea/

No comments:

Post a Comment